Tshabalala bado aiota Yanga SC

BURUDANI - - HABARI - Na ATHANAS KAZIGE

MLINZI wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ bado ameendelea kuiota Yanga, baada ya kusema kama Jonas Mkude asingetolewa kwa kadi nyekundu, wapinzani wao wangefia Uwanja wa Taifa.

Beki huyo maarufu pia kwa jina la Zimbwe Jr akizungumza na BURUDANI jana, alisema Simba iliwazidi sana Yanga kutokana na kuwasoma mbinu zao mapema na kujua jinsi ya kuwamaliza.

“Unajua kocha wetu (Joseph Omog) aliwasoma Yanga mbinu zao na kipindi cha pili, tuliingia kwa kufanyia kazi maelekezo yake ndio tukasawazisha bao, huku tukiwa pungufu,” Tshabalala.

Alisema pia kamwe hawezi kumsahau mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma kutokana na kumfanyia madhambi kila mara kwenye mchezo huo.

Mpambano wa Simba na Yanga, ulifanyika katika dimba la Taifa, Dar es Salaam ambapo timu hizo zilifungana bao 1-1.

“Ngoma anacheza rafu sana, si pekee yake. Unajua tulipowazidi ujanja, walianza kucheza faulo kwa makusudi kutaka kutuumiza, mimi nimetoka nachechemea siku ile,” alisema Tshabalala.

Beki huyo kutokana na uhodari alioonyesha Simba msimu uliopita na huu, klabu hiyo imemzawadia gari aina ya Raum.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.