Kall Ongala achimba mkwara

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

KOCHA wa Majimaji, Kally Ongala amewataka wachezaji wake kuongeza bidii uwanjani ili waweze kufanya vizuri katika mechi zijazo za msimu huu wa ligi kuu Tanzania Bara.

Akizungumza juzi, Kally alisema wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kufahamu jukumu lao ni kubwa katika michuano hiyo.

Alisema kuwa kupoteza mechi dhidi ya Stand United, kunasababisha uchungu kwa wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

“Lazima wachezaji wangu wabadilike, wajitume ili tuweze kusonga mbele, vinginevyo hali itakuwa mbaya zaidi,” alionya kocha huyo.

Tayari kikosi cha Majimaji kimepoteza mechi zote saba walizocheza msimu huu, kitu ambacho kimeanza Kally na uongozi wa klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Ruvuma (FARU), Golden Sanga alisema hivi karibuni kuwa walikutana kujadili mwenendo wa timu hiyo na kuweka mikakati kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zijazo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.