Ngasa kuinoa Toto Africans

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa timu ya Toto Africa ya Mwanza, uko mbioni kumrejesha Athuman Bilal kuwa kocha mkuu wa timu hiyo huku msaidizi wake akiwa Khalfan Ngasa.

Taarifa iliyopatikana jana, ilieleza kuwa uongozi wa timu hiyo ulikutana juzi kujadili nani atachukua mikoba baada ya aliyekuwa kocha wao, Rogatian Kaijage kujiuzulu.

Kocha huyo alijiuzulu baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Ndanda FC ya Mtwara, wiki iliyopita katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Baadhi ya wanachama, wapenzi wa timu hiyo walimfuata kocha huyo baada ya mchezo huo na kumtaka abwage manyanga, kitu ambacho alikifanya.

Hii si mara ya kwanza Bilal kurejea Toto, lakini pembeni anatarajiwa kusaidiwa kwa karibu na Ngasa ambaye ni kiungo wa zamani wa timu ya Pamba na timu ya taifa, Taifa Stars.

Ngasa ni baba mzazi wa kiungo Mrisho Ngasa anayesakata soka la kulipwa nchini Oman baada ya kuvunja mkataba wake na timu ya Free State ya Afrika Kusini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.