Wanamitindo kuchangia waathirika Kagera

BURUDANI - - HABARI -

WANAMITINDO ambao ni mabalozi wa Hifadhi za Taifa, wanatarajiwa kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera hivi karibuni kwa kuendesha hafla maalumu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mratibu wa hafla hiyo kutoka Tanzania Role Model, Samwel Malugu alisema, warembo hao 17 watashiriki katika hafla hiyo ya aina yake, itakayofanyika katika ukumbi wa Msasani Tower karibu na Hospitali ya CCBRT, kesho kuanzia saa 2 usiku huku watu maarufu wakitarajiwa kushiriki.

Malugu alisema, kaulimbiu katika hafla hiyo ni ëTanzania Yetu, Utalii Wetuí na watu walioguswa na hilo wanaombwa pia kuhudhuria kwani hakutakuwa na kiingilio.

ìTunaomba Watanzania washiriki katika hafla hii, lengo kubwa ni kushirikiana na wenzetu ambao wamepata matatizo kutokana na tetemeko hili.

ìWanamitindo hawa ambao wanawakilisha hifadhi zetu za taifa, pia wanatumia fursa hiyo ya vipaji waliyonavyo ili kuchangia waathirika wa Kagera.

Malugu alisema kuwa watakaojitokeza watapata fursa pia ya kutembelea hifadhi za Saadani na Mikumi, ambazo zina vivutio vingi vya aina yake na safari hiyo itakuwa ya bure.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.