Simba, Azam zapigwa marungu

BURUDANI - - HABARI - NA VICTOR MKUMBO

KLABU ya Simba imepigwa faini ya sh. milioni tano, baada ya mashabiki wake kufanya vurugu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba imepigwa faini hiyo na Kamati ya Bodi ya Ligi,Uendeshaji na Usimamizi baada ya mashabiki wa klabu hiyo kungíoa viti kwenye uwanja huo katika mchezo dhidi ya Yanga.

Simba na Yanga zilitoka sare bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Jumamosi iliyopita.

Mashabiki wa Simba walianza kungíoa viti na kurusha uwanjani kwa madai ya kutokubaliana na uamuzi wa aliyekuwa mwamuzi wa mchezo, Martin Saanya na kusababisha uharibifu mkubwa.

Kufuatia vurugu hizo, serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, imezifungia Simba na Yanga kutumia uwanja huo katika mechi za ligi kuu msimu huu.

Serikali ilitoa adhabu hiyo ili kuwa kuwa fundisho kwa klabu hizo kongwe nchini kutokana na mashabiki wake kurudia vitendo vya vurugu kila mara zinapocheza.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema kamati hiyo ya saa 72, ilikutana juzi na kutoa adhabu kwa Simba ya kulipa faini.

Lucas, alisema kamati hiyo katika kikao chake imelaani na kuonya vitendo vya klabu ya Simba vilivyofanywa na mashabiki wake na endapo vitaendelea adhabu zaidi itatolewa ikiwa ni kucheza bila mashabiki kwa mujibu wa kanuni ya42(3) na 24(7) za ligi kuu.

Alisema pia Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amepigwa faini sh. 200,000 kutokana na kuingia uwanjani baada ya mchezo kinyume na utaratibu kwa kuwa hakuwa kati ya maofisa wa mchezo waliotakiwa kuingia kwenye eneo hilo.

Wakati huo huo, Azam imepigwa faini ya sh. milioni 3 kwa kosa la kuvaa nembo ya mdhamini wa ligi hiyo mkono mmoja badala ya miwili ambapo ni kinyume na kanuni ya 13(1) na adhabu itatolewa kwa mujibu wa kanuni ya 13 (6).

Simba inatarajiwa kuteremka tena uwanjani Jumamosi wiki hiikuivaa Prisons katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.