Duh! Mastaa wa kikapu Bongo wafupi sana

BURUDANI - - HABARI - NA DEUSDEDIT UNDOLE

KOCHA wa mabingwa wa Taifa wa mpira wa Kikapu kwa wanawake Tanzania Bara, timu ya Don Bosco Lioness, Mohammed Yusuph amesema matokeo mabaya kwa timu yake kwenye mashindano yanayoendelea ya Kanda ya Tano Afrika, yanachangiwa na wachezaji wake wengi kuwa wafupi.

Mashindano hayo msimu huu yalianza kuchezwa Oktoba Mosi na yatamalizika kesho kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Yusuph alisema jana kuwa hatua hiyo inawafanya iwe vigumu kwa timu yake kupata ushindi katika mechi nyingi ambazo tayari timu yake imecheza.

“Ni kweli tumefanya vibaya katika mechi zetu tatu za awali. Hilo limechangiwa na vimo vifupi vya wachezaji wangu,” alisema Yusuph.

Mechi tatu za awali ambazo timu yake imepoteza ni zile dhidi ya UCU ya Uganda, TPA na U.S.I.U ya Kenya.

Akizungumzia hatima ya mabingwa hao kwenye mashindano hayo msimu huu, alisema hakuna maajabu kwani mechi zilizosalia ni chache ikilinganishwa na ambazo tayari wamecheza.

Kocha huyo wa Don Bosco Lioness, alisema kikubwa anachofurahishwa nacho ni wachezaji wake kutozidiwa ufundi na mbinu za mchezo, isipokuwa tofauti pekee tu ufupi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.