SIMBA INAPIGA TU!

HAKUNA CHA USHEMEJI WALA NINI MBEYA CITY YALIWA 2-0 AJIBU, KICHUYA WANATISHA

BURUDANI - - MBELE - NA MWANDISHI WETU

SHANGWE za Kichuya, Kichuya, Kichuya na Simba hii inapiga tu iwe ndani au nje, kwa maana ya Dar es Salaam ama mkoa wowote, zilisika jana kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati timu yao iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City.

Ikicheza kwa kujiamini katika uwanja wa ugenini, Simba ilipachika mabao yake dakika ya sita na 34 kupitia kwa Ibrahim Ajib na Shiza Kichuya.

Katika mchezo huo, Simba ilianza kwa kasi huku ikionyesha kuhitaji ushindi wa mapema baada wachezaji wa timu hiyo kufanya shambulizi kali dakika ya pili.

Shambulizi hilo lilionyesha kiu ya timu hiyo na kusababisha kasi zaidi ya mchezo ambayo ilizaa matunda baada ya Ajib kuucheza kwa ustadi mkubwa mpira wa adhabu ndogo uliojaa moja kwa moja wavuni.

Dakika ya 14 Simba ilipata penalti baada ya Rajab Zahir kufanya madhambi, lakini penalti iliyopigwa na Fredric Blagnon, ilijaa mikononi mwa kipa wa Mbeya City.

Simba iliendelea kufanya mashambulizi makali na dakika ya 28 na 32 ilipata nafasi za kufunga kupitia kwa Ajib na Kichuya, lakini mipira iliyopigwa iliokolewa na mabeki wa Mbeya City.

Mbeya City licha ya kuwa katika dimba la nyumbani, ilionekana kushindwa kuhimili mikikimiki ya Simba pamoja na kushambulia sana kipindi cha pili.

Dakika ya 49, Raphael wa Mbeya City alipiga faulo iliyomgonga usoni kipa Vicent Angban na mabeki wa Simba wakaokoa. Simba nao walipata nafasi ya kufunga dakika 55 ambayo haikuzaa matunda, ambapo iliendelea kukosa dakika ya 63 kupitia kwa Ame Ali ‘Zungu’ aliyechukua nafasi ya Blagnon.

Hata hivyo, kipindi cha pili hakikuwa na msisimko sana kwani timu zote zilicheza kwa tahadhari huku Simba ikijipanga zaidi kuzuia hatari zote langoni mwake.

Kutokana na matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 20 baada ya kushu- ka dimbani mara nane na kuendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo.

Nahodha wa Simba Jonas Mkude alisema maandalizi waliyofanya yameiwezesha timu yao kufanya vyema katika mchezo. Alisema kuwa timu yake itaendelea kujipanga zaidi na kufanya vyema katika michezo ijayo.

Hilo ni pambano la kwanza Simba kushinda nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwani ilicheza mechi saba bila ya kwenda mikoa mingine kuzikabili timu pinzani.

Kwa ushindi huo Simba imeonyesha kuwa haina uwanja ambao inacheza kwa masiraha kwani licha ya kucheza katika mkoa wa Mbeya anakotoka rais wao, Evans Aveva, haikutazama hilo badala yake iliacha kipigo hicho jana.

Kutokana na Kichuya kufunga bao amezidi kujichimbia katika usukani wa wafungaji baada ya kufikisha mabao sita, huku Ajib akitupia manne na kulingana na Amis Tambwe wa Yanga.

ISSA Rashid ‘Baba Ubaya’ wa Mtibwa Sugar, akimiliki mpira huku Tanzania Bara, uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.