Kigogo Simba atoboa siri ya mafanikio

BURUDANI - - HABARI -

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, amesema kikosi chao cha msimu huu kina mbinu nyingi za kupata ushindi katika ligi kuu ya Tanzania Bara ndio maana kinatoa dozi kwenye kila mechi.

Akizungumza jana kutoka mkoani Mbeya, Kaburu alisema kuwa wamejipanga vyema msimu huu ili kuhakikisha Simba inarejea katika heshima yake kama zamani na kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

Alisema kuwa mbinu hizo ni pamoja na mazoezi ya nguvu kila mara ili wachezaji wawe fiti kabla ya kupambana na timu pinzani, kitu ambacho amesema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kaburu pia alisema kuwa mbinu nyingine ni kuwaandaa wachezaji kisaikolojia kabla na baada ya mechi ili waweze kukubaliana na matokeo yoyote kama ambavyo walianza kufanya katika mechi dhidi ya Yanga Oktoba Mosi, mwaka huu.

“Siku ile baada ya Jonas Mkude kutolewa, tuliwaomba viongozi wa benchi la ufundi wawaeleze wachezaji wetu watulie na kipindi cha pili walitulia na kufanya kazi nzuri ikiwemo ya kusawazisha bao,” alisema Kaburu.

Alitaja mbinu nyingine ambayo wameanza kuitumia msimu huu ni kuwahi katika vituo ambavyo wamepangiwa kucheza ili kuanza kuzoea uwanja kabla ya kucheza mechi kama walivyofanya Mbeya ambako walikwenda siku tatu kabla ya mtanange huo na kufanikiwa ‘kuikong’oli’ na kuzoa pointi zote tatu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.