Azam FC yanasa 26

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

BENCHI la ufundi linaloongozwa na mtaalamu wa kuvumbua vipaji, Tom Leg kutoka Uingereza, limefanikiwa kunasa wachezaji chipukizi 26 katika mazoezi yaliyoendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaam na Tanga.

Akizungumza na BURUDANI, Ofisa Habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, alisema wamewapata wachezaji hao wadogo katika mazoezi yanayoendelea kufanyika hapa nchini ili kusaka vipaji.

Wachezaji hao wamepatikana katika mazoezi yaliyofanyika Wilaya za Temeke ambapo walipata wachezaji watano, Ilala wachezaji sita na Kinondoni watano.

Alisema mkoani Tanga wamepata wachezaji 10 ambapo jumla yao ni 26, zoezi hilo litaendelea tena katika mikoa mbalimbali na visi- wani Zanzibar ambapo watakwenda Oktoba 16, mwaka huu.

Idd alisema lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuhakikisha Azam inakuwa na kikosi bora siku zijazo, ambapo wanasaka vipaji vya vijana chini ya umri wa miaka 17, lengo hilo limeanza kufanyiwa kazi toka Agosti 28, mwaka huu ambapo walianza wilaya za Kigamboni na Temeke kwenye Uwanja wa Chamazi.

Septemba 3, mwaka huu majaribio hayo yalifanyika kwenye Wilaya ya Ilala ambapo ungíamuzi wa vipaji hivyo ulifanyika kwenye viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kuhamia kwenye Uwanja wa Kawe.

Vipaji hivyo, vitasakwa katika mikoa mingine ya Morogoro, Arusha, Mwanza na Kigoma na kwa mujibu wa ofisa huyo, wakipatikana wachezaji itaundwa timu moja kwa ajili ya kuendelea kuwachuja.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.