Owino aula Oman

BURUDANI - - HABARI - NA ATHANAS KAZIGE

UONGOZI wa klabu ya Stand United uko kwenye hatua ya mwisho kumuuza beki wao, Joseph Owino kwa timu ya Fanja ya Oman.

Taarifa iliyopatikana jana na kuthibitishwa na kocha msaidizi wa Stand, Athuman Bilal, ilieleza kuwa mchezaji huyo amefuzu majaribio baada ya kwenda nchini humo hivi karibuni.

Owino alirudi nchini juzi na jana alitarajiwa kumalizana na viongozi wa Stand ili kupewa baraka za kwenda kujiunga rasmi na timu ya Fanja kushiriki ligi kuu ya Oman.

Beki huyo raia wa Uganda, amewahi kucheza timu za Simba, Sofapaka ya Kenya anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kuanzia kesho kwenda Oman kwa ajili ya kuanza kuitimukia timu yake mpya katika michuano mbalimbali inayo ikabili.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.