Julio unajua Mwadui wanahaha kisa wewe?

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

SIKU chache baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kubwaga manyanga, uongozi wa klabu hiyo umeanza mchakato wa kutafuta kocha mpya.

Akizungumza na BURUDANI, jana, katibu mkuu wa klabu hiyo, Ramadhan Kilao, alisema kwamba wameamua kuanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine baada ya Julio kukataa kuendelea nakibarua chake.

Kilao alisema awali walifanya mazungumzo na Julio na kumsihi aendelea kuifundisha timu yake, lakini alikataa.

Alisema baada ya Julio kukataa wameamua kutafuta makocha wen- gine na tayari wameanza kupokea maombi ya makocha ambao wameonyesha nia ya kutaka kibarua hicho.

Kiongozi huyo alisema licha ya kupokea baadhi ya majina, milango bado ipo wazi kwa makocha wengine na mara baada ya kufunga milango ya kupokea maombi, watachuja majina na kuchagua kocha atakayekuwa na sifa na vigezo wavitakavyo.

“Tumeona tumwache Julio aende kwani amekataa kubadilisha msimamo wake hivyo kocha yeyote mwenye sifa tunamkaribisha kuomba nafasi,” alisema Kilao.

Julio alibwanga manyanga wiki mbili zilizopita kwa madai ya kukerwa na mwenendo wa waamuzi kwa kushindwa kuchezesha kwa haki na kufuata sheria 17 za soka.

ìNimeamua kuchukua maamuzi magumu japo kuna watu watahuzunika na wengine watashangilia kujiuzulu kwangu ila hilo halinipi shida kwa sababu siwezi kuendelea kuvumilia vitendo vya waamuzi ambao wanafanya kazi kwa ajili ya kumkomoa mtu,” alisema Julio.

Aliongeza kwa kusema ameiacha familia yake Dar es Salaam na kwenda kufanya kazi Shinyanga, lakini badala ya kupata matunda ya kazi yake watu wengine wanamharibia hivyo ni bora akae nyumbani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.