Pluijm: Siwapendi wachezaji hawa

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

KOCHA mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, amesema anawachukia wachezaji ambao wamekuwa wakicheza michezo isio ya kiungwana kwa lengo la kuwaumiza wenzao. Akizungumza na

BURUDANI, Pluijm alisema kwa muda mrefu amekuwa akichukizwa na tabia ya wachezaji hao hivyo ameona ni vyema kuweka bayana jambo hilo.

alisema kitendo hicho kina- paswa kukemewa na kuangaliwa kwa makini na waamuzi ili matendo kama hayo yasitokee mara kwa mara.

“Nasikitika kuona kila siku wachezaji si wa timu yangu pekee bali hata timu nyingine wakiumia kwa sababu ya wachezaji wachache, ambao hufanya rafu za makusudi,” alisema Pluijm.

Kocha huyo alisema vitendo visivyo vya kiungwana katika soka vinaua vipaji vya wachezaji wengi pia vinashusha maendeleo ya soka la Tanzania.

Kauli ya kocha huyo imekuja siku chache baada ya mshambuliaji wake, Amis Tambwe kuumizwa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Licha ya Tambwe, wachezaji wengine wa Yanga wanaouguza majeraha ni mabeki Andrew Vicent ‘Dante’ na Juma Abdul ambao waliumia katika mchezo dhidi ya Azam FC.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.