Kichuya kuendeleza rekodi yake leo

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

LEO ndio leo katika Uwanja wa Uhuru jijini, Dar es Salaam wakati Simba watakapokuwa wenyeji wa Mbao FC katika pambano la ligi kuu ya Tanzania Bara.

Katika mchezo huo ambao Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza na pointi 23, watacheza kwa kasi ili wazidi kuikimbia Yanga Stand United zilizopo nyuma yake. Lakini, kikubwa katika mechi hiyo ni kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya kuendeleza rekodi yake ya kucheza na nyavu na kutoa mapande kwa wenzake kuiwezesha Simba kuzidi kupepea katika usukani wa ligi.

Mpaka sasa Simba haijafungwa mechi yoyote na inakutana na wageni Mbao FC katika mtanange unaotarajiwa kuwa wa kukata na shoka baada ya timu hiyo ya Mwanza, kuzinduka hivi karibuni. Ukiacha Kichuya ambaye ndio habari ya mjini kwa sasa ndani ya Simba na ligi kuu kwa ujumla akiwa amecheka na nyavu mara saba na kuongoza kwa wafungaji mabao, kocha msaidizi wa vinara hao wa ligi kuu, Jackson Mayanja, alisema amekiandaa vyema kikosi chake kwa ajili ya kuvuna pointi tatu mbele ya Mbao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.