Nyota Simba ajiweka sokoni

BURUDANI - - HABARI - NA MWANDISHI WETU

NYOTA wa zamani wa timu ya Simba na Mbeya City, Haruna Moshi ‘Boban’, amesema yupo tayari kusajiliwa na timu yoyote katika dirisha dogo. Boban ambaye ameachana na Mbeya City msimu huu, alisema sasa yeye ni mchezaji huru na yupo tayari kujiunga na timu yoyote inayohitaji huduma yake. Mchezaji wa nafasi ya kiungo aliyewahi pia kutamba Coastal Union ya Tanga, alisema timu itakayokuwa na mkataba mnono hatasita kujiunga nayo. Boban alisema kuwa soka ni kazi yake hivyo hana budi kuangalia riziki sehemu nyingine kwa kuwa bado kiwango chake bado kipo juu licha ya kutowika kama zamani. Aliongeza kwamba milango ipo wazi na anakaribisha mazungumzo kwa klabu yoyote ambayo itamhitaji.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.