Yanga mpelampela, Chirwa azidi kutakata

BURUDANI - - HABARI - NA ATHANAS KAZIGE, MWANZA

NYOTA ya mchezaji wa kimataifa wa Yanga, Obrey Chirwa, imezidi kung’ara, baada ya jana kufunga bao katika mchezo dhidi ya Toto Africans. Mchezaji huyo wa kimataifa wa mbia, amefikisha mabao mawikatika michuano ya Ligi Kuu nzania Bara msimu huu. Mshambuliaji huyo alifunga bao kwanza katika mchezo wa jana kika ya 28 kwa mpira wa kichwa, unganisha krosi ya kiungo wa mbeni, Simon Msuva. Chirwa, aliondoa nuksi baada kufunga bao lake la kwanza katimchezo walioshinda mabao 3-1 di ya Mtibwa Sugar. Yanga jana ilitoka uwanjani kifua ele kwa ushindi wa mabao 2-0, opata kwenye Uwanja wa CCM umba, Mwanza.

Awali, mashabiki wa Yanga walipaza sauti wakidai kuwa Chirwa ni mzigo, baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza licha kununuliwa kwa bei mbaya.

Kocha Mholanzi Hans Van Der Pluijm, alimpanga, Hassani Kessy, kucheza nafasi ya beki wa kulia kujaza nafasi ya majeruhi, Juma Abdul.

Kessy, amekuwa nje ya uwanja muda mrefu, baada ya kuibua mzozo mkali baina ya Yanga na watani wao wa jadi Simba zikimgombea.

Lakini, jana aliziba vyema pengo la Abdul, baada ya mara kwa mara kuanzisha mashambulizi upande wa kulia.

Abdul, aliumia kifundo cha mguu katika mchezo uliopita dhidi ya Azam, waliotoka suluhu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Beki huyo wa kulia, aliyepigwa kwanja na Daniel Amoah, alishind- wa kuendelea na mchezo huo na nafasi yake ilijazwa na Mbuyu Twite.

Dalili za Yanga jana kupata ushindi zilionekana mapema, baada ya Simon Msuva kukosa bao dakika ya sita akiwa ndani ya eneo la hatari.

Chirwa, aliitoka ngome ya Toto Africans dakika ya 16, lakini shuti lake lilitoka nje kidogo ya lango.

Dakika ya 18 Yanga nusura ipate bao ambapo mshambuliaji, Donald Ngoma, aliingia ndani ya eneo la hatari na kuachia shuti liliokolewa na mabeki wa Toto Africans.

Toto Africans ilijibu shambulizi dakika ya 24 langoni mwa Yanga na Waziri Junior, alipata nafasi nzuri na kuachia shuti kali lililotoka nje kidogo ya lango.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu na dakika ya 46 Yanga ilipata faulo, lakini Kessy alipiga juu.

Toto Africans ilifanya shambu- lizi langoni mwa Yanga dakika ya 50 baada ya Jamal Soud kuchonga krosi murua ambayo iliokolewa na beki Vincent Andrew.

Yanga ilipata bao la pili dakika ya 55 lililofungwa na Msuva kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki wa Toto Africans kumfanya madhambi, Deus Kaseke.

Dakika ya 87 Yanga ilifanya shambulizi la kushtukiza ambapo Kessy aliachia shuti kali kipa akapangua mpira ukamkuta Chirwa na kupiga shuti nje.

Toto Africans ilijibu shambulizi dakika 88 ambapo Yusuph Mlipili aliachia shuti kali lililodakwa na kipa David Kisu.

Toto Africans iliendelea kulisakama lango la wapinzani wao na dakika ya 90 Waziri aliachia shuti kali kipa akapangua ikawa kona ambayo haikuzaa matunda.

Yanga imefikisha pointi 18 ikishinda michezo mitano kati ya tisa iliyocheza. Ilishinda dhidi ya African Lyon mabao 3-0, iliilaza Majimaji 2-0, iliichapa Mwadui 2-0 kabla ya kuifumua Mtibwa Sugar 3-1.

Pia ilitoka sare ya bao 1-1 na Simba, ilitoka Suluhu ilipovaana na Ndanda kabla ya kulala bao 1-0 dhidi ya Stand United, ilitoka suluhu na Azam kabla ya jana kuichapa Toto Africans. Toto Africans: David Kisu, Yusuph Amosi, Salum Chuku, Carlos Protas, Yusuph Mlipili, Ramadhani Malima, Jamal Soud, Reliaut Lusajo, Waziri Junior, Wiliam Kimanzi na Jafari Mohammed.

Yanga: Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassani Kessy, Oscar Joshua, Vincent Andrew, Kelvini Yondani, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.