MAN UTD INATISHA AISEE

Dimba - - Mbele - >>24

IKIWA ugenini katika dimba la Vitality, timu ya Manchester City imefanikiwa kujihakikishia nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth jana.

Ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Everton, City chini ya Guardiola ilifanikiwa kuzinasa pointi tatu hizo muhimu shukrani kwa mabao yaliyowekwa kimiani na Gabriel Jesus dakika ya 21 akisawazisha bao la Charlie Daniels lililopachikwa dakika ya 13 ya mchezo. Raheem Sterling ndiye aliyefunga la ushindi kwa upande wa City.

United nayo iliichapa Leicester City mabao 2-0 katika mtanange uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford. Mabao ya United yaliwekwa nyavuni na straika Marcus Rashford, aliyepachika bao hilo dakika chache baada ya kutoka benchi kipindi cha pili, akiunganisha vyema kona iliyochongwa na Henrikh Mkhitryan, asisti ya tano msimu huu kwa Muarmenia huyo.

United ikapata bao lake la pili zikiwa zimesalia dakika nane mpira umalizike, akigusa kidogo tu shuti lililopigwa na Jese Lingard, na kuifanya timu hiyo ishinde mchezo wake wa tatu wa awali katika ligi bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa, ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2005/06.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.