Umesikia sarakasi za Chirwa Yanga?

Dimba - - Mbele - NA CLARA ALPHONCE

BAADA ya sintofahamu juu ya usajili wa Straika kutoka Ghana, Nicolaus Gyan, hatimaye mchezaji huyo anatarajia kuwasili nchini Agosti 31, Alhamisi tayari kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mghana huyo anarejea nchini wakati timu yake ikianza vizuri michuano ya Ligi Kuu, ambapo jana iliimwagia mvua ya mabao 7-0 Ruvu Shooting na kuongoza katika msimamo wa ligi.

Gyan ambaye anatokea katika timu ya Ebusua Dwarfs ya Ghana, alitambulishwa kwenye tamasha la Simba Day lililofanyika Agosti 8 jijini Dar es Salaam, alirejea nchini kwao siku ya pili baada ya kumalizana na Simba.

Wakala wa mchezaji huyo, Juma Ndambile, aliliambia DIMBA kuwa, mchezaji huyo ni halali wa Simba baada ya kuingia nao mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

“Mchezaji huyo aliingia mkataba na Simba wakati bado ana mkataba na timu yake, hivyo kama Simba wangembakiza Tanzania kwa ajili ya mechi yao na Yanga, ilibidi wanunue mkataba wake.

“Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi huu, hivyo tukaona haina haja kwa kuwa muda uliobaki ni mdogo, ni bora arudi kwao akamalizie mkataba wake na baadaye arejee akiwa mchezaji huru,” alisema Ndambile.

Ujio wa mchezaji huyo unaweza kuongeza kasi ya upachikaji mabao katika kikosi cha Simba, ambapo hivi sasa nafasi hiyo inashikiliwa vizuri kwa ushirikiano wa Emmanuel Okwi, Juma Luzio, Mohamed Ibrahim, Laudit Mavugo na Mzamiru Yassin.

Nicolaus Gyan

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.