MO amzuia Ndemla kwenda Ulaya

Dimba - - Jumapili - NA MWANDISHI WETU

SIKU chache baada ya kuwapo kwa taarifa ya kiungo wa Simba, Said Ndemla, kutimkia Ulaya kucheza soka la kulipwa, inaelezwa kuwa mfadhili wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘MO’, amesimamisha mpango huo akitaka aitumie klabu hiyo.

Taarifa za ndani zilizonaswa na DIMBA, zinadai kuwa tajiri huyo ndiye aliyewazuia wachezaji wengine wa timu hiyo, Laudit Mavugo na Shiza Kichuya waliokuwa na mpango wa kutimkia St George ya Ethiopia pamoja na Shiza Kichuya aliyepata nafasi ya kucheza soka nchini Misri.

“MO hataki kusikia habari za kuondoka mchezaji kipindi hiki cha ligi kuu hasa kutokana na matokeo mazuri waliyoanza nayo wachezaji wa Simba,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Ndemla alikataa kuzungumzia juu ya safari yake na kudai kwamba wakala wake, Jamal Kisongo, ndiye anayeelewa kila kitu na yeye kazi yake ni kucheza soka tu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.