Stand United waanza ligi Kuu kwa neema

Dimba - - Jumapili - NA MAREGES NYAMAKA

NI kwa neema. Hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wa timu ya Stand Unite kupata udhamini wa Sh milioni 10 kwa mwaka kutoka Kampuni ya Michezo ya Bahati Nasibu (BIKO).

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Ellyson Maeja, amesema ni jambo la faraja kufanikisha udhamini huo kwani umekuja kwa wakati ambapo watazitumia kwa maendeleo ya timu na si vinginevyo.

“Tunawashukuru BIKO kwa uungwana wao waliounyesha kuja kuweka udhamini wao mahali hapa, tunawaahidi hatutawaangusha, soka la kisasa liko hivyo duniani kote,” alisema Maeja.

Aliongeza kuwa wadhamini hao watakuwa wanatoa motisha kwa kila mchezo ambao Stand United itakuwa inaibuka na ushindi sambamba na wafungaji wa mabao hayo, ingawa hakuwa tayari kubainisha ni kiasi gani.

Wapiga debe hao jana walishuka uwanjani kuwavaa Mtibwa Sugar, katika Dimba la Manugu Complex, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwao wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18 ambapo Stand walipoteza kwa bao 1-0.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.