Matola: Tshishimbi ni mtu hatari sana

Dimba - - Jumapili - NA JESSCA NANGAWE

KOCHA Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola, amesema wanaingia dimbani wakiwa na tahadhari ya kumchunga zaidi kiungo mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi, kwani ameonekana ni mchezaji hatari sana.

Akizungumza na DIMBA, Matola alisema wamejiandaa vyema kukabiliana na timu yoyote watakayokutana nayo licha ya uchanga wa kikosi hicho kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Aliongeza kuwa hawaangalii ukubwa wa timu wanayokwenda kupambana nayo kwa kuwa kila timu imejipanga vyema kuhakikisha inashinda, huku akiwatahadharisha wachezaji wake kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo wanapokuwa uwanjani.

“Tunakwenda kupambana na Yanga, nadhani ni timu itakayotupa ushindani mkubwa ukizingatia wana wachezaji wazuri, tumejipanga kupambana nao na tutacheza kwa tahadhari kubwa, lakini wakiwa na ingizo jipya la Tshishimbi ambaye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ameng’ara sana,” alisema Matola.

Katika heshima nyingine, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo wa leo na majeruhi waliokuwa kwenye kikosi chao wanaendelea vyema, hivyo huenda wakawatumia katika michezo ya hivi karibuni.

Wachezaji waliokuwa majeruhi ni pamoja na Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya, Beno Kakolanya pamoja na Hamis Tambwe.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.