Mieleka waomba mechi kuahirishwa

Dimba - - Jumapili -

CHAMA cha Mchezo wa Mieleka Tanzania (AWATA), kimeomba kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa timu ya Taifa ya mieleka dhidi ya Burundi, zikiwa ni mechi za makundi kwenye mashindano ya Afrika.

Akizungumza na DIMBA, Kaimu Katibu Mkuu wa AWATA, Eliakim Merkizedeki, alisema wamelazimika kuandika barua pepe kwa Chama cha Mieleka Barani Afrika kuomba usogezwe mbele mchezo huo ili kupisha hekaheka za uchaguzi wa Awata uliopangwa kufanyika Septemba 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Kwa sasa kila kiongozi akili zake amezielekeza kwenye uchaguzi mkuu, hivyo ni vigumu kuandaa timu ya taifa itakayokuwa na ushindani,” alisema.

Katika mashindano ya Afrika mwaka huu, timu ya Tanzania imepangwa katika kundi B lenye timu za Burundi, Kenya, Rwanda, Ethiophia na Shelisheli.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.