Young Dee ajutia kumkana mwanae

Dimba - - Jumapili - CLARA ALPHONCE

RAPA anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Bongo Bahati Mbaya’, Young Dee, amesema baada ya kukaa na kutafakari ameona ni kweli alikosea kwa kitendo chake cha kumkataa mwanaye kwa mara ya kwanza na kuomba jamii imsamehe.

Akizungumza na DIMBA, Young Dee alisema maamuzi ya kumkataa mwanae huyo yalichangiwa na maisha magumu aliyopitia enzi za utoto na sasa yeye ni baba mzuri anayemhudumia mtoto wake kwa mapenzi yote.

“Nadhani ule ulichangiwa na utoto, najutia sana maamuzi niliyoyafanya kwa sababu yalikuwa ya ghafla, mashabiki zangu waelewe tu nilijikwaa bahati mbaya na sasa nimejielewa, kwa sasa ninamlea mtoto wangu na anapata mapenzi yote na kila kitu,” alisema Young Dee.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.