Idris Sultan kuzindua viatu vyake

Dimba - - Jumapili - NA JESSCA NANGAWE

MSHINDI wa Big Brother 2014, Idris Sultan, anatarajia kuzindua viatu vyake sokoni kesho alivyovipa jina la SultanXForemen ambavyo vitakuwa ni vya kiume pekee.

Akizungumza na DIMBA, Idris alisema atazindua viatu hivyo ambayo vitakuwa vikipatikana katika maduka mbalimbali jijini Dar es salaam na kwenye baadhi ya mikoa.

“Uzinduzi wangu utaambatana na kuanza kuvisambaza kwenye maduka mbalimbali ambayo tumeingia nayo mikataba, lengo hasa ni kuhakikisha bidhaa zetu zinakubalika ndani na nje ya Tanzania,” alisema Idris.

Alisema viatu hivyo vina ubora wa hali ya juu na amezingatia ubora ili kuwapa watu kilicho bora.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.