Shapovalov afuzu ku shiriki US Open

Dimba - - Jumapili -

MKALI wa tenisi kutoka Canada, Denis Shapovalov, ameteka vichwa vya habari mara baada ya kufuzu kucheza mashindano ya US Open kwa kupata ushindi wa seti 6-7(2), 6-1, 6-3 dhidi ya Jan Satral.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, yupo katika kiwango bora hivi sasa ambapo katika michezo 17 ya mwisho amepoteza miwili pekee.

"Seti yangu yangu ya kwanza nilipoteza jambo lililofanya nikose amani," Shapovalov alikiambia kituo cha ATPWorldTour.com.

"Kiukweli imenipa motisha na imenisaidia kunifanya nijiamini. Lakini seti ya pili ilinirudisha mchezoni na nikaanza kujiona naweza kuibuka na ndivyo ilivyokuwa katika seti ya tatu ambayo ndiyo iliyoamua matokeo.

"Inashangaza nilikuwa na ndoto ya kucheza mashindano haya makubwa ambayo kila mchezaji wa tenisi anatamani kucheza Grand Slams, ni jambo la kuvutia na heshima kwangu,” alisema.

Wamarekani wote watatu wataanza kurusha karata yao katika hatua ya awali, Smyczek atafungua dhidi ya Sam Querrey, King akianza na seed Pablo Carreno Busta huku Aragone akianza kutafuta heshima dhidi ya seed Kevin Anderson.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.