JATA KUSHIRIKI UCHAGUZI IJF

Dimba - - Jumapili - NA ZAINAB IDDY

RAIS wa Chama cha Mchezo wa Judo Tanzania (Jata), Khalifa Kiumbemoto ‘Chief Kiumbe’, anatarajia kuondoka nchini Agosti 28, mwaka huu kwenda Hungary kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mchezo huo (IJF) uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Mbali na uchaguzi huo wa kuwapata viongozi wapya wa IJF, lakini pia utatanguliwa na mkutano mkuu kwa wanachama wa shirikisho hilo.

Akizungumza na DIMBA, Katibu Mkuu wa Jata, Innocent Mallya, alisema msafara wa Rais wa Judo Tanzania upo chini ya IJF watakaogharamia suala usafiri, chakula pamoja na malazi kwa kipindi chote cha siku tatu atakazokuwa Hungary.

“Rais wa Jata ataondoka sambamba na wale wanamichezo wawili wanaokwenda kushiriki mashindano ya dunia nchini Hungary Agosti 30, mwaka huu.

Mallya alisema akiwa huko rais wa Jata atapata fursa ya kuzungumza na viongozi mbalimbali ili kupata wadhamini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.