Harmonize: Nimefunga ukurasa wa Wolper

Dimba - - Jumapili - NA JESSCA NANGAWE

MKALI wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wasafi Classic, Harmonize, amesema kwa sasa amefunga ukurasa wa kuzungumzia habari za mpenzi wake wa zamani, Jackline Wolper kwa kuwa walishamalizana. Hivi karibuni Wolper aliamua kufunguka undani wa kuachana kwao, huku akidai chanzo kikubwa ni baada ya Harmonize kumsaliti kwa kuwa na mwanamke mwingine bila yeye kujua. Akizungumza na DIMBA, Harmonize alisema aliamua kuachana na Wolper kwa sababu ambazo zilikuwa na uzito wake na kuendelea kuzungumzia jambo hilo ni kupoteza muda kwa kuwa ana mambo mengi ya kufanya. “Kuendelea kuzungumzia mambo yaliyopita ni kupoteza muda kwa sababu tulishafunga ukurasa huo, kikubwa kwa sasa tufanye kazi na maisha yaendelee, sitakaa nizungumze habari hizo tena,” alisema Harmonize.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.