YAMOTO BILA MIL. 30 HAWAPANDI JUKWAANI

Dimba - - Jumapili - NA GLORY MLAY

MSANII wa Bongo Fleva, Bakari Katuti almaarufu Beka Fleva ambaye ni mmoja wa wasanii kutoka Yamoto Band, amesema bila Sh milioni 30 kundi hilo haliwezi kufanya shoo sehemu yoyote.

Akizungumza na DIMBA, alisema kundi lao likifanya shoo bado mashabiki watataka wasanii hao waimbe mmoja mmoja, kitu ambacho kinawagharimu sana.

“Kama kundi bila Sh milioni 30 hatupigi shoo, kwa sababu tukipanda jukwaani tukiimba kama kundi mashabiki watataka mimi niimbe nyimbo zangu, watamtaka na Asley naye aimbe, kitu ambacho kitatugharimu kutokana na kwamba tunafanya shoo ya kuwa ndege wawili kwa jiwe moja,” alisema.

Alisema kwa sasa hawatafanya shoo za Sh milioni 10 kama walivyozoea, hivyo aliwatka waandaji shoo kujipanga kwa suala hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.