Nyimbo mpya ya Swift gumzo

Dimba - - Jumapili -

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Taylor Alison Swift, amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii nchini humo mara baada ya kuachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Look What You Made Me Do’ ambacho kimewagusa maelfu ya mashabiki wake.

Nyimbo hiyo ambayo ipo kwenye albamu mpya ya mwanadada huyo aliyoipa jina la ‘Reputation’, amekuwa akipokea pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki wake kutokana na ujumbe uliopo katika kibao hicho.

Huu umekuwa mwanzo mzuri kwa Swift mwenye umri wa miaka 27 ambaye anatarajia kuachia albamu yake ya sita mwaka huu.

Mkali huyo wa kibao cha You Belong With Me, anatamba na albamu nyingine kama vile Tailor Swift aliyoiachia mwaka 2006, Fearless(2008), Speak now (2010), Red (2012) pamoja na 1989 (2014) ambazo bado zinaendelea kufanya vizuri sokoni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.