Golovkin, Canelo waingia anga za Derevyanchenko

Dimba - - Jumapili -

BINGWA wa uzito wa kati raia wa Ukrain, Serhiy Derevianchenko, amemwambia meneja wake kuwa hivi sasa anataka kupanda ulingoni na mmoja kati ya Golovkin na Canelo ambao wamekuwa wakitajwa kuwa mabondia bora hivi sasa.

Bondia huyo raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 31 ambaye ana rekodi ya (12-0,3 ,9 KO), ameyasema hayo mara baada ya kupata ushindi wa KO dhidi ya Tureano Johnson ambao ni ushindi wa 12 tangu alipoanza kucheza masumbwi.

“Nipo tayari kupanda ulingoni na mshindi kati ya Golovkin vs. Canelo ili nigombee nao mkanda, hivi sasa naamini hao ndio levo yangu.

“Nafikiri Golovkin atashinda pambano hilo, naamini ndiye nitakayepanda naye ulingoni katika pambano langu lijalo,” alisema.

Ulikuwa ushindi mzuri dhidi ya Johnson na ulikuwa mwanzo mzuri kuelekea katika pambano langu lijalo ambalo litachezwa mwisho wa mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.