NYOTA ZETU

Dimba - - Jumapili - Utabiri huu unaandaliwa na Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki, Ramadhani Yahya, anatibu maradhi na matatizo ya kidunia anapatikana kwa simu namba 0652 545462, Makao Makuu Magomeni Kagera, jijini Dar na Hale, mkoani Tanga.

SIMBA (LEO) JULAI 23-AGOSTI 23

Unatakiwa kuheshimu ugeni uliokuwa nao nyumbani, vilevile yapo matatizo yatakayokusumbua akili yako, siku za Jumapili unaweza kuzitumia kutafuta kukamilisha masuala yaliyokukatiza.

MASHUKE (VIRGO) AGOSTI 23-SEPTEMBA

Wasiwasi ulionao ni wa kujitakia huna sababu ya kuhangaika mambo yako sasa yameiva na yatakuja bila kutumia nguvu nyingi, mpango unaoufikiria utahitaji muda wa ziada na uaminifu wa kutosha ili ufanikishe.

MIZANI SEPTEMBA 24-OKTOBA 23

Utasikia habari njema lakini hutofanikisha ulichopanga, yupo mtu usiyemtarajia atakueletea taarIfa ya matumaini, acha dharau sikiliza kila ushauri huu ni wakati wa kupata mambo mengi ya muhimu kutoka kwa watu mbalimbali.

NGE (SCROPION) OKTOBA 24-NOVEMBA 22

Utapokea taarifa njema siku ya Alhamisi, ipokee na kuiacha hivyo hivyo ni mtego unaoweza kukupeleka sehemu mbaya, lipo jambo ulilolianza na kukwama sasa litafufutuka na kuleta mafanikio unaweza kupata ushauri wa kinajimu kwa msaada zaidi.

MSHALE (SAGITARIUS) NOVEMBA 23-DESEMBA 21

Kuna hali ya kuugua au kuuguliwa na mtu unayemtegemea suluhisho ni wewe jaribu kujiweka karibu na familia, mali na heshima vinakuja hivi punde acha kushirikisha watu usiowajua vizuri katika mambo yako ya siri.

MBUZI DESEMBA 22-JANUARI 20

Furaha uliyopata itaendelea kuwepo uvumilivu ndiyo silaha yako, endelea kujiweka wazi katika mambo yako kufichaficha mambo itakugharimu, punguza hasira ili uaminike na kupata faida, kuna mtu unayemdanganya naye anajua unachofanya.

NDOO JANUARI 21-FEBRUARI 19

Ni wiki nzuri kutembelea jamaa na kupata mawazi mapya ni wakati wa kusogea katika maisha usikae pekee na kujifungia zipo riziki za kutosha, utakutana na myu atakushauri biashara au wazo la kupata kipato usilidharau pia epuka uvivu utakaouhisi sana wiki hii.

SAMAKI FEBRUARI 20-MACHI 20

Utasifiwa kwa kufanya jambo fulani, faida nayo itakuja endapo unafanya biashara au kazi, unatakiwa kusaidia familia yako hasa nduguyo anayeumwa hii itakuongezea baraka ya kupata mambo zaidi, siku za Jumanne utapata habari mpya.

PUNDA MACHI 21-APRIL 20

Kuna jambo umelifanya bila kujua lakini bado uliyemtendea anakukumbuka wiki hii utakutana naye na kushangaa mtakavyopanga mambo muhimu, uwe makini endapo utahitaji kuingia katika masuala mapya ya mapenzi.

NG'OMBE (TAURUS) APRILI 20- MEI 21

Ni wiki unayotakiwa kuishi kwa kuwa mwangalifu sana, vinginevyo utapata hasara utajuta, wapo watu wanaokufuatilia kuharibu mipango yako, kwa wafanyabiashara wanaweza kufanikisha mipango yao siku za Jumamosi tu.

MAPACHA (GEMINE) MEI 21-JUNI 21

Utasikia jambo litakalokukosesha amani hata hivyo bado aibu yako itaendelea kuwa siri usipende kuzungumzia mambo yako muhimu na mtu usiyekuwa na uhakika naye jiepushe pia makundi usiyoyatambua vizuri.

KAA (CENCER) JUNI 21-JULAI 23

Utapata kishawishi fulani huenda ukaingia katika hatua nyingine ya maisha, mafanikio sasa yanakukaribia ondoa vikwazo vya kifamilia uanze kuonja mafanikio, habari watakazotaka kukuzushia hazitakuharibia mipango yako.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.