DIAMOND, KING KIBA

Wakumbusha ya Tupac, Notorious

Dimba - - Jumapili - NA MWANDISHI WETU

BIFU ni msemo maarufu sana wenye maana ya chuki iliyozidi kipimo.

Hiyo ni maana ya haraka haraka lakini inayogusa pande zote za maisha ya binadamu. Mara nyingi wanaochochea chuki hizo huwa ni watu wa pembeni, yaani wapambe.

Inaingia kwenye sehemu nyingi lakini Sanaa ndiyo iliyotekwa zaidi na huo msemo. Kiuhalisia, bifu si kwamba ni kitu kibaya katika maisha ya kila siku. Ni jambo la kawaida hasa kwa washindani kuamsha mikwaruzano ya hapa na pale. Na mara kadhaa tumewaona wanamuziki wakiwa ndio wahusika wakuu kwa kuzozana. Hawa ndio wanaobeba maana kubwa ya bifu. Tunapozungumzia bifu kali zilizoteka katika historia ya muziki duniani, hatuwezi kuyaacha majina kama Tupac Shakur na Notorious B.I.G.

Ni rahisi sana kwa Ja Rule kurudi kwenye gemu ya muziki na kumpiku Diddy kwa kipato kuliko wapenzi wa muziki kusahau bifu la Tupac na B.I.G.

Awali walikuwa ni marafiki wakubwa tu. Ila baadaye wakaja kutofautiana na 2Pac akamshutumu B.I.G kwamba alihusika na tatizo lake la kwanza kabisa lililosababisha asogezwe mbele ya vyombo vya sheria.

Hapo sasa ngoma zenye mistari kwenzi na ‘diss’ za kutosha zikaanza kurekodiwa, mijadala motomoto ikaibuka baina ya wadau mbalimbali wa muziki. Ikafika mbali zaidi kwa 2pac kupigwa risasi baada ya kipindi kifupi na kufariki. Ilielezwa kwamba kufeli kwa moyo baada ya zile risasi nne alizomiminiwa ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya kifo chake.

Baadaye B.I.G naye akatandikwa risasi na waliohusishwa sasa ni wale wa upande wa pili, yaani wa 2Pac ambao walikuwa wakijiita ‘West Coast’. Ndipo ulimwengu wa muziki ukaja kugundua kuwa bifu la washkaji halikuwa la kitoto. Na uadui baina ya East na West Coast usingeisha mapema.

Bifu halikuishia huko mamtoni tu, likafika hadi kwetu Tanzania na wengi wetu tutayakumbuka mabifu ya wanamuziki wetu wa Bongo Fleva miaka ya nyuma.

Dudubaya na Mr. Nice hadi kufikia kupigana, bifu la Sister P na Zay B kipindi hiko wako kwenye chati vibaya mno.

Bifu la wasanii wa TMK Wanaume na wale wa East Coast Team. Hadi ilifikia hata shoo ya wale wa East Coast kurushiwa mawe na wahuni wa Temeke kipindi fulani.

Inspekta na Juma Nature, Nako 2 Nako na mkongwe Afande Sele na O Ten ambao bifu lao lilikuwa gumzo kidogo. Historia nimekupa ili upate mwanga wa machache nitakayosema pengine msingi wake uwe kwamba bifu kwenye muziki.

Kikubwa kilichonifanya niandike hili ni kuhusu ngoma mpya mbili za vinara wa Bongo fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba. Wikiendi hii, wawili hawa wameachia ngoma zao, Diamond akitoka na ‘Zilipendwa’, huku Kiba akiibuka na kibao cha ‘Seduce me’.

Tuanze na Diamond. Ni moja ya kazi zake nzuri ambazo zimekubalika haraka sana na wadau wake wa muziki muda mfupi tu baada ya kuiachia.

Hicho ndicho wadau walichokitaka. Na si kutupiana maneno mengi mitandaoni kiasi cha kuvunjiana heshima na wengine kujikuta wakifanya yale ambayo wao wenyewe hawapendi kufanyiwa.

Swali moja tu la kuwauliza hawa wasanii wetu ambao wana utajiri mkubwa sana, tena sana wa mashabiki hapa Tanzania na nje ya nchi.

Je, wanataka kufikia yale ya Dudubaya na Mr. Nice kutwangana? Au kufika mbali zaidi hadi kupoteza maisha na tuanze kuhisi timu hii au team wale wamehusika? Ni ushamba.

Kama ni msanii mmoja katoa au kashirikishwa katika ngoma na kumdiss mwenzake, kumjibu kwa ngoma kali si mbaya. Ndivyo muziki unavyokuzwa.

Lakini, kwa yaliyotokea hapa katikati kabla ya ‘Zilipendwa’ kutoka ni aibu na hatutaki kuona yakitokea tena. Hakuna cha kujifunza pale, ukweli na usemwe.

Diamond umegusia kipande cha bifu la Mr. Nice na Dudubaya kuwa ni ‘Zilipendwa’. Safi sana. Ila bifu za kitoto tunahitaji kuona huu uwe ndio mwisho wake kuanzia sasa.

Kwa upande wa Kiba, ngoma ya ‘Seduce me’ imetikisa kwelikweli. Ndani ya masaa 14 baada ya kutoka na kuwekwa kwenye mtandao wa YouTube, ilipata watazamani ‘viewers’, zaidi ya laki tatu.

Si kitu rahisi kutokea katika siku za hiv karibuni.

Hii ilikuwa na maana gani kwa Kiba? Ra hisi sana. Mashabiki walimmisi ‘King’ wao kama wanavyopenda kumuita. Ulipita mwaka mmoja tangu walipousikia wimbo wake wa mwisho, nauzungumzia ‘Aje’.

Maswali kibao yameibuka kwa wadau wa muziki tangu Kiba aachie ngoma hiyo, siku chache tangu aingie kwenye vita baridi ya maneno na mkali mwingine wa Bongo Fleva Diamond Platinumz.

KWANINI AMETOA NYIMBO BAADA YA KUGOMBANA NA DIAMOND?

Hili linaweza lisiwe na majibu sahihi kwa sasa, lakini ukweli ni kuwa King Kiba alikuwa na mpango wa kuachia ngoma mpya kabla hata malumbano ya kimtandao hayajaanza.

Alishatoa ‘teaser’ mbalimbali akiashiria kuwa yuko mbioni kuachia ngoma mpya, huku wengi wakibashiri kuwa ngoma hiyo ingeitwa Kipusa, lakini ghafla Kiba, akaachia ‘Seduce me’.

Huenda pia malumbambo yake na Dia mond, yaliongeza hamasa ya kuachia ngoma yake mpya kwa kuwa tayari alishateka vichwa

vya watu kwa mijadala mitandaoni.

VIPI UBORA WA NYIMBO?

Ukiisikiliza kwa makini ngoma ya ‘Seduce me’, utagundua kuwa wimbo ule upo kwenye mahadhi ya RnB ‘Rhythm and blues’.

Kwa kipindi kirefu soko la Bongo Fleva limekosa ladha za muziki wa aina hiyo na inavyoonekana Ali Kiba ameamua kutumia mwanya huo ili kukosha nyonyo za mashabiki wake.

Lakini hii pia inaweza kuwa silaha ya siri ya Kiba katika ramani ya muziki wa Bongo Fleva. Kwanini? Si wasanii wengi wenye uwezo wa kuimba muziki aina ya RnB, hivyo anajaribu kuutumia ili kuteka soka akijua atakuwa peke yake na kushusha wengine wasioweza staili hiyo ya muziki.

Wadau wa muziki nao wamempongeza Kiba kwa uwezo wake wa kuimba muziki unaoweza kupenya hata katika soko la kimataifa na kubeba tuzo, zinazosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Bongo Fleva.

MASHABIKI WANASEMAJE?

Uko upande unaoonyeshwa kutoridhishwa na wimbo huo na upo upande unaotoa pongezi kwa King Kiba kwa kutoa ngoma kali iliyokata

kiu

yao ya muda mrefu. Kama nilivyosema awali, mahadhi ya wimbo wa ‘seduce me’ si rafiki sana na masikio ya Wabongo wengi waliozoea kuruka staili za viduku, hivyo inahitaji muda kidogo na kazi kubwa kufanyika ili Kiba aweze kuliteka jumla soko la muziki nchini

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.