PANGA PANGUA X1 INAWAHUSU

Dimba - - Jumapili - NA MAREGES NYAMAKA

P AZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara lilifunguliwa rasmi katikati ya wiki hii kwa mechi ya Ngao ya Jamii iliyoikutanisha miamba ya soka nchini, Simba na Yanga na mtanange kumalizika Wekundu wa Msimbazi kuibuka kidedea kwa kutwaa taji hilo.

Katika mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu, ulikuwa na sura mpya za wachezaji waliopiga kazi haswa uwanjani.

Jina la kiungo mpya wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, limekuwa maarufu zaidi kwa kudhihirisha ubora wake ndani ya dimba la kati kwa kuunganisha timu vema kuwalinda mabeki wake pamoja na katikati kwenda mbele.

Hilo lilidhihirika hata kwa upande wa mashabiki wa upinzani Simba, kukubali ufundi wa mchezaji huyo kuwa alikuwa kikwazo kwao kupata matokeo ikiwamo kocha wao Joseph Omog.

Mbali na gumzo la Mcongo huyo ambaye takwimu zake zinaonyesha alikuwa kinara wa kupiga pasi 51 zilizofika kwa mlengwa, makala hii inakuletea nyota wengine wapya vikosini humo walioonyesha ukomavu mkubwa na huenda wakafanya balaa kubwa msimu huu.

ERASTO NYONI

Beki wa kushoto wa Simba, Erasto Nyoni, alionyesha ushupavu wa hali ya juu namna ya kukaba, kupokonya mipira kupandisha timu na kupiga krosi nyingi sahihi ambazo hazikutumiwa vyema na mastraika Laudit Mavugo na Emmanuel Okwi.

Ingizo hilo jipya la Mnyama hadi anafanyiwa mabadiliko na benchi la ufundi, nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alikuwa amepiga jumla ya krosi sahihi saba, akipokonya mipira kwa adui mara mbili.

Utulivu wa kupandisha timu na kurejea kwenye eneo lake kwa wakati sahihi akikaba kwa nidhamu, iliwanyima kabisa akina Rafael Daudi, Emmanuel Martin na Juma Abdul uhuru wa kukokota mpira kwa muda mrefu wala kupiga krosi.

Kulingana na utimamu wake wa mwili muda mrefu tangu akiwa na timu yake ya zamani Azam, ana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Omog akiwa kama mchezaji tegemeo.

Wachezaji wanaocheza beki za pembeni kushoto na kulia, watarajiwe kuwa na wakati mgumu akina Ally Shomari, Jamali Mwambeleko na Shomari Kapombe, amamekuwa baye akikumbwa n a majeraha ya mara kwa mara.

Gadiel Michael ampia baye alimweka benHajji chi Mwinyi dakika zote 90 za mchezo, ilikuwa furaha nyingine kwa mashabiki wa Yanga kutokana na kutimiza majukumu yake vilivyo.

Uwezo wake wa kukaba ngadu kwa ngadu ulimwezesha kumfanya mpinzani wake wa upande huo Shiza Kichuya asisogee sana kwenye eneo la hatari kupiga krosi hatarishi langoni, wala yale mashuti ya moja kwa moja kwenda langoni kama ilivyozoeleka.

Hata ilipotokea Kichuya anabadilishana na Niyonzima kwenda upande huo, bado Gadiel alikuwa mtulivu wa kuzima zile heka heka za Niyonzima kutengeneza pasi.

Kitendo hicho cha kuwabana wawili hao kulimfanya

kubaki nyuma kuliko kupandisha timu mara kwa mara na kwa kupiga zile krosi zake kama ilivyozoeleka. Takwimu zinaonyesha hadi mpira unamalizika alikuwa amepiga krosi tatu pekee zote zikiwa fyongo, mbili zikipita juu ya lango na mpira ukitoka nje ya uwanja sambamba na kushindwa kutengeza nafasi hata moja. Katika mchezo wake wa leo wa ligi ambao kikosi chake kitachuana na Lipuli ya mkoani Iringa chini ya kocha mzawa Seleman Matola, winga Salum Machaku na wenzake wanatakiwa kuwa na mbinu mbadala za kumtoka beki huyo.

SALUM MBONDE

Mbonde alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza muunganiko mzuri kati yake na nahodha Methodi Mwanjali, wakizima makali yote ya mastraika hatari wa Yanga, Donald Ngoma na Ibrahim Ajib.

Zao hili la Mtibwa, mara nyingi alikuwa anabaki ‘kumaki’ inapotokea Mwanjali amesogea mbele kuanzisha mashambulizi hadi mpira unamalizika alikuwa amepokonya mpira mara nne kutoka miguuni mwa Ngoma pamoja na Ibrahim

Ajib. Huku akicheza asilimia nyingi ya mipira ya vichwa iliyokuwa ikielekezwa langoni mwao na kuwafanya wapinzani wao kuambulia patupu.

AISHI MANULA

tofaukatika imekuwa pia na prewa mashabiki.

Lakini mtihani huo taratibu unaanza kumwepuka Manambaye alidatimu yake mechi kwanza dhidi ya watani wa jadi kwa kikubwa kwa vishindo kugeuka

Wachezaji wengi wapya wameshindwa kuendeleza ubora ndani ya Simba na Yanga ti na walikotoka vikosi vyao, ikichangiwa sha ya wingi ula kia ya

akifanikiwa kiasi kuhimili na ghafla kuwa kipenzi cha wana Msimbazi.

Hatua hiyo inamfanya piga ua kuwa chaguo la kwanza la Omog katika kikosi cha kwanza cha kudumu na kuwachomesha mahindi katika benchi akina Said Mohamed ‘Nduda’ na Emmanuel Mseja ambaye ni chaguo la tatu.

Nidhamu ya mchezo na uzoefu mkubwa katika michezo ya kimataifa akiwa na Azam FC, pamoja na timu ya Taifa, Taifa Stars, ni silaha yake kubwa kuwagopesha hata mastraika wa timu pinzani.

Takwimu zinaonyesha mechi dhidi ya Yanga alikuwa ameokoa hatari tatu langoni ‘save’ pamoja na kupangua penalti ya kwanza ya beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondan.

IBRAHIM AJIB

Kama ilivyo kawaida yake hachezi mpira wa mabavu sana kama ilivyo akina Donald Ngoma, lakini ni hatari anapoanza kukokota mpira akiliangalia lango la mpinzani nje ya eneo la hatari, ingawa katika mchezo na timu yake hiyo ya zamani alibanwa vilivyo na mabeki wa Simba.

Pamoja na kutoonyesha kiwango cha juu ni ngumu sana kwa kocha wake George Lwandamina kutomjumuisha katika kikosi cha kwanza kuanzia leo mchezo dhidi ya Lipuli ambapo aina ya timu kama hizo mabeki ambao hawajawahi kucheza naye ana asilimia kubwa ya kuwafanyia balaa hasa la upigaji wa mipira.

Ingizo hilo jipya la Mnyama hadi anafanyiwa mabadiliko na benchi la ufundi, nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alikuwa amepiga jumla ya krosi sahihi saba, akipokonya mipira kwa adui mara mbili.

Ibrahim Ajib Erasto Nyoni Aishi Manula

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.