Adebayor Nimeitwa Togo kwa sababu maalumu

Dimba - - Jumapili -

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor, amesema ameitwa kwenye kikosi hicho kwa sababu maalumu ikiwemo kuhakikisha timu hiyo inapata mafanikio. Adebayor amesisitiza kwamba yeye bado ana uwezo mkubwa, hivyo imani aliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba anaisaidia timu yake kupata mafanikio zaidi, lakini kurejesha makali ya Togo katika ngazi ya kimataifa.

"Tupo kwenye mazingira bora hivyo tunachokihitaji ni kuirejesha Togo katika makali yake kimataifa, tunaamini kwamba ushirikiano wetu utasaidia kulifanya Taifa letu kuwepo katika heshima yake.

Kocha wa Togo, Claude Le Roy, amesema ameita kikosi imara kwa ajili ya kulitetea Taifa katika mechi mbili muhimu za kirafiki.

Togo inatarajia kuwa mwenyeji wa Niger katika mchezo wa kirafiki Agosti 31, mwaka huu kisha kukutana Septemba 4, mwaka huu dhidi ya Malawi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.