Free State yatimua kocha

Dimba - - Jumapili -

KLABU ya Free State Stars imemfukuza kocha wake, Sammy Troughton, baada ya kuiongoza kwenye mechi mbili katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini (Absa) katika msimu mpya wa mwaka 2017/18.

Free State imeshindwa kueleza sababu hasa za kumfukuza ingawa wadadisi wa mambo wanasema kwamba chanzo ni kutoridhishwa na uwezo wa Troughton katika mechi hizo pamoja na zile za kujipima nguvu kabla ya msimu kuanza.

Mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo, Ea Lla Koto, amethibitisha kuchukua maamuzi ya kumtimua kocha huyo ingawa hawakueleza sababu za msingi.

Troughton alijiunga na Free State wakati wa maandalizi ya ligi msimu huu, huku uongozi ukiwa na imani kwamba anaweza kufanikiwa kupata mafanikio kwenye ligi msimu huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.