Mabondia ngumi za ridhaa waanza kujifua kwa Madola

Dimba - - Jumatano - NA ZAINAB IDDY

JUMLA ya mabondia 25 wa ngumi za ridhaa, wakiwamo wanawake 10, wameanza maandalizi ya michuano ya Jumuiya ya Madola, itakayofanyika Aprili, mwakani nchini Australia.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga, ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, mabondia hao chini ya kocha wao, John Mwakipesile, wanafanya mazoezi katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Alisema kufanya mazoezi pia wamewawekea programu ya kucheza mapambano ya kujipima nguvu, ili kujiweka na Jumuiya ya Madola ambapo mabondia watakaokwenda kuiwakilisha nchi ni wale watakaoonyesha kiwango kwenye michezo ya kirafiki watakayopigana.

Mkurugenzi wa Kampuni ya GF Trucks Equipment, Imran Karamal (kushoto), Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala (katikati) na Mwenyekiti wa timu ya Mbao FC, Soly Njashi, wakitambulisha jezi zitakazotumiwa na timu hiyo baada ya kampuni hiyo kutangaza...

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.