Kamodee akimbiza mashindano ya Gospel

Dimba - - Jumatano -

NA JESSCA NANGAWE

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Kamodee Mali ya Mungu, amejihakikishia kuibuka mshindi katika mashindano ya Gospel Kanda ya Ziwa, yanayotarajiwa kufikia tamati Jumapili hii.

Akizungumza na DIMBA, Kamodee, ambaye ni miongoni mwa washiriki wa shindano hilo, alisema anamshukuru Mungu, kwani mpaka sasa ameendelea kushika nafasi ya kwanza kwa kufikisha kura zaidi ya 18,000 na ana matumaini ya kuibuka mshindi.

Mashindano hayo yameandaliwa na Radio Ukumbozi, yanashirikisha jumla ya waimbaji 16, ambao wanapigiwa kura kwa lengo la kumpata mshindi wa Kanda hiyo.

ìMimi nitawakilisha Kanda ya Ziwa na wimbo wangu wa 'Ameniona Mungu' na mpaka sasa nashukuru watu wameendelea kunisapoti kwa kunipigia kura, nawaomba waendelee kufanya hivyo hadi siku ya mwisho ili niweze kuibuka mshindi,î alisema Kamodee.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.