JUMA ABDUL: Kipaji chake ni biashara na mapishi ya kila aina

Dimba - - Jumatano -

NAJULIKANA kwa jina la Juma Abdul, ni beki wa kulia wa timu ya Yanga, Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara 27.

Uwezo wake wa kusakata soka ndio umemfanya kujulikana na wapenzi wengi wa soka hapa nchini.

Amesajiliwa Yanga akitokea timu ya Mtibwa Sugar na huu ni msimu wake wa tano kuitumikia klabu hiyo, yenye maskani yake Mtaa wa Twiga na Jangwani, Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

DIMBA imeamua kuzungumza na mchezaji huyo ili kuweza kujua maisha yake ya kawaida akiwa uraiani yakoje na amekuwa akiishi vipi na majirani zake na marafiki kwa ajumla.

Unajulikana sana kwenye maisha ya soka, katika maisha ya kawaida unajichanganya vipi na watu?

Nikiwa mtaani naishi kama kawaida kama Juma Abdul, ambaye anaishi maisha ya kawaida anayotakiwa kuishi mwanadamu yeyote, sina makuu.

Unaishi wapi na nani, kwa ujumla familia yako ikoje?

Naishi Kimara na mchumba wangu. Familia yangu ni ya kawaida.

Unaishi na mchumba, lini

DIMBA: ABDUL:

DIMBA: ADBUL: DIMBA:

unatarajia kufunga naye ndoa?

Muda si mrefu kuna vitu bado naweka sawa.

Unapenda kuishi maisha gani, ya ustaa ama ya vipi?

Hapana, maisha ya kawaida ambayo hayamkwazi mtu.

Unapenda kula chakula gani?

Ugali, samaki au nyama ya kukaanga, mlenda na kachumbari.

Unajua kupika chakula chochote?

Ndiyo, najua kupika vyakula vyote, iwe biriani, pilau, ugali, wali, makande na kadhalika, na sababu kubwa iliyonifanya nijue kupika ni marehemu baba yangu kipidi cha uhai wake alikuwa anapenda sana tujue kupika, kwani alikuwa anatuambia katika maisha kuna leo na kesho, hivyo hatuwezi kila siku tuwe tunakula kwa mama ntilie.

Tofauti na kupika, kazi gani nyingine za nyumbani ambazo unaweza

ADBUL: DIMBA:

ABDUL:

DIMBA: ABDUL:

DIMBA: ABDUL: DIMBA:

kufanya?

Ni kufua na kufanya usafi, huwa namsaidia mpenzi wangu kama akiwa amechoka.

Mtindo gani wa nywele ambao unapenda kunyoa, na mavazi gani ambayo unapenda kuvaa na rangi unazopenda?

Mtindo wa nywele ninaoupenda ni panki kwa sababu ndio unanipendeza.

Mavazi ninayopenda kuvaa ni jinzi na tisheti nyeupe na raba nyeupe na kama nikiwa nimevaa pensi ambayo ina mkato mzuri halafu chini nivae 'sendozi' nyeusi juu tisheti yoyote.

Marafiki zako wa karibu ni watu wa aina gani?

Mtu yeyote ambaye atanipa ushauri mzuri katika maisha, hasa mambo ya maendeleo, anayejiheshimu, si rafiki ambaye anaweza kukupoteza katika maisha.

Una kipaji gani kingine zaidi ya soka?

DIMBA: ABDUL: DIMBA: ABDUL: DIMBA: ABDUL: ABDUL: DIMBA: ABDUL:

Sina kipaji chochote, ila tu nina bahati ya biashara.

Ili uwe na hasira au furaha, mtu akufanyie kitu gani?

Ili niwe na hasira nisikie familia yangu imekosa raha kwa sababu ya mtu fulani, hasa mama yangu, wadogo zangu na mke wangu, ili niwe na furaha familia yangu ikiwa na furaha.

Katika maisha yangu mama yangu ni namba moja, nikifikiria alivyopata shida na mimi wakati baba yangu amefariki naumiaga sana kuona mtu anamnyanyasa.

Unapokuwa na mama yako kuna mambo gani anapenda kuongea na wewe, kama mzazi?

Vitu vingi, cha kwanza ananikumbusha tulipotoka na tunapoelekea, niangalie makundi na starehe hazina mwisho, nimkumbuke sana Mungu ili mambo yangu yaweze kwenda vizuri, hasa ukiangalia kipindi hiki cha ujana nilichonacho.

Siku yako haiwezi kwisha bila kufanya nini? Na msanii gani ambaye anakuburudisha zaidi?

Siku yangu haiwezi kwisha bila kusikiliza muziki, sina msanii ninayempenda sana, ila napenda mziki mzuri, lakini ukinikuta kwenye mizunguko yangu napenda sana kusikiliza kazi za Dogo Aslay.

Siku chote umaarufu haukosi changamoto, wewe unakutana na

DIMBA: ABDUL: DIMBA: ABDUL: DIMBA:

changamoto zipi mtaani kwako kutoka kwa mashabiki zako.

Mimi sijawahi kukutana na changamoto yoyote kutokana na jinsi nilivyojiweka na jinsi ninavyoishi nao.

Kitu gani huwezi kusahau katika maisha ya soka na maisha yako kwa ujumla.

Katika soka nakumbuka maisha kwa ujumla, siku nilipokuwa nikisoma Shule ya Sekondari Makongo kwa ajili ya kipaji maalumu, lakini baadaye alipoondoka Idd Kipingu ambaye alikuwa mkuu wa shule pale akaja mtu mwingine mambo yakawa mabaya na kupelekea kushindwa kumaliza shule, kwa sababu yule aliyekuwepo alikuwa hataki mambo hayo, anataka mtu ulipe ada na mimi mzazi wangu alikuwa hana uwezo, hivyo nikashindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, na hapo nikaamua kwenda Mwanza kutafuta maisha ya soka, ndipo nikapata nafasi ya kucheza katika timu ya Toto Africans.

Katika soka sitasahau siku ambayo Toto Africans ilipokuwa inataka kushuka daraja na sisi kukaambiwa lazima tuipiganie timu iweze kubaki, na ikaundwa kampeni ya kuibakiza Toto Ligi Kuu chini ya Mkuu wa Mkoa, Jamal Rwambo, mwisho tukafanikiwa kuibakiza ligi na ilikuwa furaha sana kwetu.

Kama mtu maarufu, unajiepusha vipi na usumbufu wa wanawake?

Kwa kweli changamoto hiyo ni kubwa sana kwetu, utakuta mtu anakupigia simu anakwambia anakupenda, ila inategemeana na wewe umelelewaje na unajiwekaje, kwa upande wangu huwa nawaambia mimi nimeoa.

ABDUL: DIMBA: ABDUL: DIMBA: ABDUL:

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.