Ni shabiki kindakindaki wa Man United

Dimba - - Jumatano -

NAITWA Floyd Joy Mayweather Jr raia wa Marekani(40) ambaye ni bingwa wa ngumi uzito wa Super Featherweight, akiwa amecheza mapambano 50, lakini hajawahi kupoteza hata moja, tangu aanze kupanda ulingoni na kufanya kuwa na rekodi ya aina yake kwenye mchezo huo.

Katika dondoo tano za mastaa, nyota huyo amenukuliwa kwenye jarida maarufu la Forbes, ambapo aliweza kuweka hadharani maisha yake ya ndani na nje ya uwanja. Bingwa huyo wa ubingwa wa dunia wa WBC Super Featherweight, anasema yeye ni bingwa kwa sababu ameandaliwa kuwa bingwa.

"Mimi ni shabiki wa Manchester United na nimekuwa nikihudhuria mara kadhaa mechi za Ligi Kuu ya England pamoja na michuano mingine. Nimekuwa shabiki kwa zaidi ya miaka 20 sasa, hivyo najivunia kwa sababu licha ya ushabiki wangu, lakini klabu yenyewe imekuwa ikiniheshimu kwa kunipa nafasi ya kukaa kwenye viti vya watu mashuhuri katika Uwanja wa Old Traford.

"Nilishasema kwamba nastaafu lakini niliamua kubadili maamuzi yangu baada ya kupata ofa kubwa zaidi. Kwa hiyo hata leo ikitokea amekuja promota akatoa fedha ninayoitaka nitapanda tena ulingoni.

"Oktoba 11, 1996 ndiyo siku nilipocheza pambano langu la kwanza ambalo nilimshinda Roberto Apodaca, raia wa Mexico kwa TKO. Pambano hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Texas Station, North Las Vegas nchini Marekani.

"Ni kweli katika mapambano yangu yote 50 niliyofanikiwa kucheza, nimekuwa nikipigana kwenye ardhi ya Marekani, ingawa hiyo hainifanyi nisionekane bora kwa sababu mabondia wengi nawapiga hadi kushindwa kuendelea na mchezo. Mapambano ambayo nashinda kwa pointi ni machache, vile vile waamuzi wanatoka nje ya Marekani kwa hiyo si rahisi kupendelewa kama ambavyo watu wachache wamekuwa wakiamini.

"Kwa sasa siwezi kusema hasa ni kiasi gani ninachomiliki, lakini kwa takwimu za mwaka jana, mimi ndio nilikuwa mwanamichezo wa 16 ninayelipwa zaidi duniani. Kwa ujumla niliweza kuingiza kiasi cha dola milioni 44 (zaidi ya shilingi bilioni 98 za Kitanzania). Kwenye ngumi pekee niliweza kuingiza kiasi cha dola milioni 32 (zaidi ya bilioni 71 za Kitanzania)," anasema nyota huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.