Hatima ya Chirwa, Kaseke kujulikana kesho

Dimba - - Jumatano -

NA SALMA MPELI KAMATI ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji inatarajiwa kukutana leo kwa ajili ya kupitia masuala mbalimbali, ikiwemo kesi inayowakabili wachezaji, Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Simon Msuva ambao wamesimamishwa kucheza kwa sasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Abasi Tarimba, itawahitaji wachezaji hao kwa ajili ya kwenda kutoa utetezi wao.

Alisema wachezaji hao walisimamishwa na Kamati ya Saa 72 kutokana na kufanya kosa la kumsukuma mwamuzi katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara msimu ulipita dhidi ya Mbao FC, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na suala lao kupelekwa kwenye Kamati hiyo ya Sheria kwa ajili ya kulitolea maamuzi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.