Nyota Gofu akiona cha moto mtandaoni

Dimba - - Jumatano - NA SHARIFA MMASI

BAADA ya kumalizika kwa michuano ya gofu Afrika Mashariki na Kati (Zone 5), baadhi ya mashabiki wamejitokeza na kumshambulia nyota aliyekuwa miongoni mwa wachezaji waliowakilisha nchi, Amani Said, kupitia moja ya kurasa zake za mtandao wa kijamii.

Michuano hiyo, iliyomalizika Jumamosi iliyopita Uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam, ilishirikisha jumla ya nchi sita, wakiwamo mabingwa watetezi Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.

Baada ya Tanzania kushika nafasi ya pili katika michuano hiyo, mashabiki waliingia kwenye ukurasa wa Amani na kumshambulia wakidai kwanini wamewaangusha na kuwaacha majirani zao Kenya kuchukua kombe.

Pamoja na mashabiki wa gofu kuonyesha kuchukizwa na nafasi waliyoshika Tanzania, Amani aliibuka na kuwataka wawe na imani nao, kwani watajipanga na kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza ili msimu ujao waibuke kidedea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.