MOURINHO AMPIGIA SIMU SANCHEZ

Dimba - - Jumatano -

LONDON, England KUTOKANA na uhitaji mkubwa wa Jose Mourinho kwa mchezaji anayetakiwa kusababisha hatari mbele ya boksi la wapinzani, imebidi yafanyike mawasiliano baina ya klabu ya Man United na staa wa Arsenal, Alexis Sanchez.

Sanchez, ametajwa kutokuwa na furaha kwa sasa ndani ya timu hiyo na aliomba kuuzwa juzi baada ya kichapo cha aibu cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Dirisha la usajili wa majira haya ya kiangazi linatarajiwa kufungwa kesho saa sita usiku, na katika kuhakikisha nyota huyo anasaini United, mawakala wa Sanchez wamewavutia waya United.

Hata hivyo, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, asingependa kumpoteza Sanchez lakini klabu hiyo huenda ikakubali kama zikija fedha nono mezani.

Wakati huohuo inaripotiwa kuwa Man City wako tayari kuipa Arsenal fedha na nyota wao, Raheem Sterling, ili waweze kumpata Alexis Sanchez.

Ofa hii inakuja wakati huu ambapo Alexis ameshawasilisha barua ya kuomba kuuzwa kwa viongozi wa Arsenal.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.