CCM Kirumba, Majimaji waupiga chini Uhuru

Dimba - - Jumapili - NA MAREGES NYAMAKA

KABLA ya michezo ya jana ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Majimaji uliopo mkoani Ruvuma, na ule wa CCM Kirumba, wa jijini Mwanza, ni viwanja pekee vilivyoingiza idadi kubwa ya watazamaji msimu huu kuliko viwanja vingine, ukiwamo ule wa Uhuru, unaotumiwa na Simba na Yanga.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, aliweka wazi kwamba mchezo ambao Majimaji waliwaalika Yanga Uwanja wa Majimaji na ule ambao Simba walikuwa wageni wa Mbao FC, Uwanja wa CCM Kirumba, ndizo mechi zilizoingiza mashabiki wengi.

Alisema michezo hiyo kila mmoja uliingiza mashabiki 12,000, huku akilalamika kwamba, msimu huu idadi ya mashabiki wanaoingia kwenye viwanja mbalimbali inaonekana kupungua, tofauti na msimu uliopita.

Hadi sasa uwanja ulioingiza watazamaji wengi ni Majimaji, uliopo Songea, mchezo uliochezwa kati ya wenyeji Majimaji dhidi ya Yanga, pamoja na CCM Kirumba ulipochezwa mchezo kati ya Mbao FC dhidi ya Simba, ambapo kila mechi iliingiza watazamaji 12,000,î alisema.

Baada ya Ligi hiyo kuchezwa jana, leo tena kutakuwa na mtanange mkali kati ya Stand United dhidi ya Simba, mchezo ambao nao unatarajiwa kuingiza idadi kubwa ya mashabiki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.