MAN CITY, YAICHAPA CHELSEA DARAJANI

Dimba - - Mbele - SOUSSE, Tunisia

KAMA wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mechi za soka kote ulimwenguni, basi hupaswi kukosa mechi hii kwani miamba miwili ya soka barani Afrika, Al Ahly ya Misri na Etoile du Sahel ya Tunisia itarejesha upinzani wao uwanjani pale itakapovaana katika mechi kali na ya kukata na shoka itakayozikutanisha timu hizo Jumapili hii katika dimba la Stade Olympique de Sousse, jijini Sousse, Tunisia.

Hii ni mechi ya kwanza ya nusu fainali inayozikutanisha timu hizo vigogo barani Afrika na itapigwa kuanzia saa 12:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, ambapo Al Ahly, mabingwa mara tisa wa michuano hiyo, watakuwa wakiwania kuweka rekodi ya kutinga fainali yao ya 11 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nusu fainali ya kwanza ilipigwa juzi Ijumaa usiku, ambapo USM Alger ya Algeria, ililazimishwa suluhu na Wydad Casablanca ya Morocco kwenye uwanja wa Stade du 5 Juillet.

Wydad ambao ni vigogo wa soka nchini Morocco watawakaribisha USM Alger katika mechi ya marudiano inayotarajiwa kupigwa Oktoba 20, huku ile ya Al Ahly na Etoile ikitarajiwa kupigwa Oktoba 22 mwaka huu nchini Misri.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.