Goran aisoma Simba kimya kimya

Dimba - - Mbele -

NA SAADA SALIM MSERBIA, Goran Kopunovic, anayetajwa kurejea nchini kukinoa kikosi cha Simba, amesema hata leo ataifuatilia timu hiyo itakapocheza na Stand United, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kopunovic, ambaye inasemekana anaandaliwa kuchukua nafasi ya Joseph Omog, amesema kila mchezo ambao Simba wanacheza anauangalia kupitia mtandao wa Youtube na hata wa leo pia atauangalia.

"Ni kweli naifuatilia sana Simba na hata huo mchezo wao unaokuja (leo dhidi ya Stand United) nadhani nitauangalia, kwani hiyo ni moja ya timu ninazozipenda kutokana na jinsi nilivyofanya nao kazi," alisema.

DIMBA lilipomuuliza kwamba dili lake na Simba linakwendaje, alisema yeye yupo tayari kurejea kwenye kibarua chake hicho kama viongozi watamhitaji, kwani hiyo ni kazi yake, ikizingatiwa kuwa hawakuachana kwa ubaya.

"Nasisitiza kwamba, kama wakiwahi nitakuwa tayari kuja huko Tanzania na kujiunga nao, kwani hata tulipoachana hatukuachana kwa ubaya wowote," alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.