UHURU KUIONDOA BARCELONA LA LIGA

Dimba - - Mbele - CATALONIA, Hispania

RAIS wa klabu ya Barcelona amesema kuwa huenda wangeamua ni ligi gani ya soka wangecheza kama jumuiya yao ya Catalonia ingepata uhuru kutoka Hispania.

Klabu hiyo ya Catalonia ilicheza mechi ya La Liga dhidi ya Las Palmas wikiendi iliyopita katika dimba lao la Nou Camp bila mashabiki, kutokana na mzozano uliopo baina ya Serikali ya Hispania inayotumia nguvu dhidi ya Wanacatalonia wanaotaka kupiga kura ya kuamua hatima ya upande wao.

Zaidi ya watu 840 walihitaji kufanyiwa matibabu baada ya kulumbana vilivyo na mapolisi, wakijaribu kupiga kura hizo zilizotafsiriwa na Serikali ya Hispania kuwa ni kinyume cha sheria.

“Kuhusu uhuru, klabu na wajumbe wake wangeamua ligi ya kushiriki. Tupo katika wakati mgumu na kwa yatakayotokea siku za usoni tutayapokea kwa upole na hekima,” alisema Bartomeu baada ya mkutano wa bodi ya klabu.

Wiki iliyopita, Waziri wa Michezo wa Catalonia, Gerard Figueras, alisema Barcelona inaweza kucheza katika nchi nyingine kama wataupata uhuru kutoka Hispania.

“Kama uhuru utapatikana, timu za Catalonia zilizopo La Liga: Barcelona, Espanyol na Girona zitaamua kama zitaendelea kucheza Hispania au Italia, Ufaransa au Premier League,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.