MAYAY ATETEA ‘UBUTU’ WA MABAO YANGA

Dimba - - Jumatano - NA JESSCA NANGAWE

PAMOJA na safu ya ushambuliaji ya Yanga kuonekana butu, mchambuzi wa soka, Ally Mayay, amesema imechangiwa na kocha kukosa mfumo mmoja pamoja na majeruhi ndani ya kikosi hicho.

Yanga mpaka sasa tayari imejikusanyia mabao manne na wapinzani wao wakiwa na mabao 12, huku ikiwa imecheza michezo mitano.

Akizungumza na DIMBA, Mayay amesema kwa Yanga ya sasa ni lazima kocha George Lwandamina apate tabu katika kupata mfumo mmoja kutokana na timu kukabiliwa na majeruhi ambao ni tegemeo katika timu sambamba na ujio wa wachezaji wapya.

“Ngoma hayupo fiti asilimia zote, bado ni majeruhi, ukiangalia Tambwe naye hivyo hivyo, pengo la Msuva nalo bado linaonekana, hapa lazima kocha apate tabu kidogo katika kuunda mfumo utakaoisaidia Yanga kupata mabao men-

gi, nadhani tumpe kocha muda wa kutosha ili aweze kutengeneza timu na mfumo ambao anaona utamfaa,” alisema Mayay.

Aliongeza kuwa pia kocha anapaswa kuwapa nafasi zaidi wachezaji wapya waliosajiliwa akiwemo Buswita na Rafael ambao wanaonekana kuja kuwa na mafanikio makubwa ndani ya timu hiyo.

Yanga kwa sasa inakamata nafasi ya 6 ikiwa na pointi 9 na inajiandaa na mchezo wa ugenini dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.