Msisiri yaichapa Combine

Dimba - - Jumatano - NA GLORY MLAY

TIMU ya wanaume ya kriketi ya Msisiri, imeibuka kidedea baada ya kuichapa Combine mikimbio 39-38 na mitupo 20-7, katika mchezo wa mashindano ya ligi ya watoto (Junior) uliochezwa Uwanja wa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Ligi hiyo ilishirikisha jumla ya timu 20 za wasichana na wavulana wa shule mbalimbali za msingi.

Katika mchezo mwingine, timu ya Accademy ilishindwa kutamba baada ya kuchapwa mikimbio 71-38 na mitupo 205 na Mkwawa, mchezo uliochezwa Uwanja huo huo.

Aidha, Academy Boys ilishindwa kutamba mbele ya Karume baada ya kufungwa mikimbio 53-52 na mitupo 8-4. Mbali na mchezo huo, pia Mkwawa waliweza kuibuka kidedea baada ya kuichapa Karume mikimbio 45-43 na mitupo 8-6.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.