MOBETO ambwatukia Idris Sultan

Dimba - - Jumatano - NA MWANDISHI WETU

MWANAMITINDO Hamisa Mobeto amembwatukia msanii Idris Sultan kwa kitendo chake cha kuhoji kiasi kikubwa cha pesa ya matumizi alichokuwa akipewa na mzazi mwenzake, mwanamuziki Nassib Abdul 'Diamond Platinum'.. Hamisa amewabwatukia watu hao baada ya kukerwa na posti Idriskwenye mitandao ya kijamii akimlaumu Diamond kwanini pesa zile asingezipeleka kwa watu wenye uhitaji na si kumpa mtu mmoja kwa maana ya mwanamitindo huyo. Baada ya Idris kuandika hivyo, Hamisa alimjibu na kumwambia: "Wewe ndio mtu pekee uliyekazania elfu 70 na Rav 4 kuliko hata huyo aliyetoa mwenyeweÖmtoto anapangwa na Mwenyezi Mungu na kumbuka wakati hiyo gari inatolewa haikutolewa wakati nina mimba or kisa ya mimba ilitolewa kwa mapenzi..na hiyo elfu 70 haikutolewa coz ya mtoto ilitolewa kwa mapenzi pia coz mtoto hakuwa kazaliwa... kusaidia watoto wasio na uwezo ni jambo jema tena lenye baraka...mwambie afanye hivyo bila kutumia ishu yangu na mtoto kama kigezo." Kwa mujibu wa Diamond, ambaye hivi karibuni alihojiwa na kukiri kuzaa na mwanamitindo huyo, alisema alikuwa akimpa si chini ya Sh elfu 70 kwa siku na kumnunulia gari aina ya Rav 4 kwa ajili ya matumizi yake na mtoto. Kwa sasa Diamond na mwanamitindo huyo wamekubaliana kumtunza mtoto wao, Dyalan kwa kutoa pesa za matumizi kwa kufuata sheria.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.