Jackline Wolper humwambii kitu kwa Fid Q

Dimba - - Jumatano - NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongo Movie, Jackline Wolper, amesema amekuwa akifuatilia kwa karibu kazi za msanii Fid Q na kugundua ndiye msanii pekee ambaye nyimbo zake hazichuji.

Wolper ameliambia DIMBA kwamba, amekuwa akifuatilia muziki wa Fid Q tangu msanii huyo alipoanza kuchana mistari na kamwe hajawahi kusikia nyimbo mbaya.

ìFid Q ni mtu wa kuogopwa sana na ni namba nyingine kabisa, yaani ni mtu ambaye namkubali sana, nina ngoma zake toka anaanza muziki hadi hii ya ëFresh', hakuna hata moja inayonichosha kusikiliza,î alisema Wolper.

ìHakuna wimbo wa Fid ambao siujui na ambao siupendi, napenda ngoma zake zote, sijawahi kuchukia ngoma yake hata moja na ninafikiri anatambua hilo,î aliongeza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.