Wachezaji kutoka Ligi Kuu ya visiwani Z’bar hawastahili kucheza TAIFA STARS?

Dimba - - Special -

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ilianza kutimua vumbi Agosti 26, mwaka huu, ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita ilichezwa raundi ya tatu ya michuano hiyo.

HIVI karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka visiwani Zanzibar, wakilalamikia wachezaji kutoka ligi ya huko kutopewa nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuona wachezaji wa visiwani humo hasa wale wanaocheza timu za huko, ni nadra sana kukutwa anaitwa kwenye kikosi cha Stars.

Wapo baadhi ya wadau wanadai kuwa jambo hilo lilikuwepo zamani wakati inachezwa Ligi ya Muungano lakini kwa sasa suala hilo halipo kabisa.

Ukiachilia mbali wale wachezaji wa Zanzibar wanaocheza kwenye timu za Bara kama Nadir Haroub 'Cannavaro', Agrey Moris, Haji Mwinyi, Khamis Mcha 'Vialli' na wengine ambao mara kadhaa wamekuwa wakipewa nafasi kwenye timu hiyo, lakini wale wanaotokea Ligi ya Z’bar, imekuwa ni ngumu, je, tatizo ni nini?

Ukiwa kama mdau wa soka nchini unazungumziaje suala la wachezaji wanaocheza Ligi ya Zanzibar kutopata nafasi ya kucheza kwenye timu ya Taifa Stars?

Tuma maoni yao juu ya suala hilo ukianzia na jina lako kamili na mahala ulipo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.